KATIKA
hali ya kushangaza mastaa mbalimbali na warembo nchini China wameamua
kutupia picha zao mitandaoni wakionyesha nywele zao za makwapani katika
kushiriki shindano la picha za kwapani kwa wanawake.
Mwanzilishi
wa shindano hilo, Xiao Yue anasema uzuri wa mwanamke si lazima asiwe na
nywele kwapani na kuongeza kuwa shindano hilo halimaanishi kuwa
wanawake wasinyoe nywele hizo ila nia yake ni kuondoa dhana potofu kuwa
nywele hizo hazikubaliki kwa mwanamke na kuonekana jambo la aibu kwa
wenye tabia ya kuziacha..
Mshindi
wa shindano hilo atakayekuwa ametokelezea na kujiamini atapata zawadi
nono katika shindano hilo lililoanza Mei 26, mwaka huu.
Mtandao
wa Weibo umejaa picha za warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo
litakalomalizika Juni 26, mwaka huu wakiwa na furaha kuinua mikono yao
juu na kuonyesha makwapa yao yenye nywele kwa dunia nzima.
0 comments:
Post a Comment