Ni
mwezi mmoja umebaki kufikia siku nyingine kubwa kwa Watanzania kupiga
kura kumchagua Rais wanaemtaka, Wabunge pamoja na Madiwani kwenye
Uchaguzi mkuu utakaofanyika October 25 2015.
Tayari
mpaka sasa tumeona Mastaa mbalimbali wa Tanzania ambao hawajaficha
hisia zao ni nani wanamkubali zaidi kwenye kumpa uongozi wa nchi na
nafasi nyingine zinazogombaniwa.
Mwimbaji staa wa bongofleva Ali Kiba ameungana
na mastaa wengine kama Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Steve Nyerere,
Aunty Ezekiel, Ray ‘Vicent Kigosi’ na wengine kuiunga mkono CCM na
mgombea wake Urais ambaye ni Dr. John Pombe Magufuli.
Pamoja
na kwamba Ali Kiba ameonekana kwenye headlines za kampeni za CCM,
hakuwahi kuandika au kupost chochote kwenye kurasa zake kuhusu kiongozi
gani anaeona ni sahihi kwake ila sasa ndio amefanya maamuzi hayo kwa
mara ya kwanza.
Credit: Millardayo

0 comments:
Post a Comment