Mtoto
aliyezaliwa akiwa na kichwa kikubwa. Dokta Agricore aliyasema hayo
alipokutana na MC maarufu jijini Dar, Joyce Amina Mwakipunda ‘Mc Jojo’
na Mtangazaji wa Kipindi cha Tashtiti Zetu cha Redio Uhuru, Nuru Issa,
walipofika hospitalini hapo kutoa misaada mbalimbali kama vile pampasi,
mafuta, poda, maji ya kunywa, juisi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku
yao ya kuzaliwa.
Ugonjwa
unaowakabili watoto waliotoka mgongo nje pamoja na vichwa vikubwa,
unaelezwa kusababishwa na ukosefu wa Folic Acid mwilini, hali
inayochangiwa na mama mjamzito kupenda kula chipsi kuku.Daktari wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wodi ya watoto ya Moi, Agricore Joseph
alisema wanawake wengi hufikia hatua ya kujifungua watoto wenye matatizo
hayo kutokana na kupenda vyakula hivyo, kitu ambacho kinaweza
kuepukika.
Mtoto
akiwa na uvimbe mgongoni. “Nakujua wewe ni MC maarufu, huko unakopita
jaribu kuwaelimisha wanawake juu ya tatizo hilo, na wewe Nuru kwenye
kile kipindi chako waelimishe wanawake juu ya hili, naamimi tunaweza
kupunguza idadi ya wanaojifungua watoto wenye tatizo hili,” alisema
daktari huyo.Alisema, ni wakati sasa wanawake hasa wajawazito
kuelimishwa juu ya kutopendelea chipsi kuku badala yake kutumia vyakula
ambavyo vinaongeza Folic Acid na kunywa vidonge vinavyotolewa kliniki.
0 comments:
Post a Comment