Polisi wakiwasambaratisha vijana wanaosadikiwa wa Chadema huku vijana hao wakiwatrushia polisi Mawe.
|
Vijana
wanaosadikiwa kuwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleov Chadema
wamevunja Mkutano wa Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi
jimbo la Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha. Tukio hilo limetokea leo
katika kata ya Rau mtaa wa rau Madukani.
Jeshi la Polisi wakiwa wamemtia nguvuni baadhi ya vijana waliokua wakileta fujo.
|
Katika
tukio hilo Mh. Davis Mosha alikua na Mkutano wa kampeni katika kata
hiyo ya Rau ndipo maandalizi ya mkutano huo yakaanza mapema Asubuhi.
Ilipofika muda wa saa tano Asubuhi lilikuja kundi kubwa la vijana
wanaosadikiwa wafuasi wa Chadema na kuanza kufunga bendera za chadema
katika eneo hilo ambalo ccm walikua wakifanya mkutano. Baada ya bendera
hizo kufungwa ndipo wanachama na viongozi wa ccm walipokuja na kutaka
kutoa bendera hizo lakini vijana hao walioonekana kupangwa kwa ajili ya
tukio hilo walipotishia iwapo bendera hizo zitashushwa basi damu
itamwagika. Kutokana na kauli hiyo huku vijana hao wakiwa wamekusanya
mawe sehemu moja ililazimu viongozi hao kuwasiliana na jeshi la polisi
ili kuweza kusimamia amani katika eneo hilo.
Mmoja wa Mwanachama wa ccm akiomba msaada baada ya kujeruhiwa kwa jiwe.
|
Baada
ya polisi kuwasili pamoja na kikosi cha kutuliza ghasia vijana hao
walianza kurusha mawe kushambulia jeshi la polisi pamoja na wanachama wa
chama cha mapinduzi waliopo katika eneo hilo. Katika mashambulizi hayo
yaliweza kujeruhi wanachama wa ccm na raia kadhaa waliokua katika eneo
hilo. Jeshi la Polisi liliweza kumkamata kijana aliyefahamika kwa jina
la Remy ambaye ndiye anayesadikiwa kuongoza kundi hilo la vijana
wanaokadiriwa kufika sitini. Kiongozi huyo wa kundi hilo amekamatwa
pamoja na wenzake wane huku wengine wakitokomea kusikojulikana.
Kiongozi wa kundi la vijana ambao hao mwenye kilemba akitoa maelekezo kwa vijana hao.
|
Davis
Mosha aliweza kuzungumza kuhusu tukio hilo alisisitiza wananchi wa
Moshi kuilinda amani ya Moshi na kuwaasa vijana kuepuka na kundi dogo la
watu ambao wana maslahi binafsi na kuwatumia katika uvunjwaji wa amani.
Vurugu hizo zimepelekea mkutano huo kuvunjika.
Kijana aliyetambulika kwa jina la Remy ambaye ndiye kiongozi wa kundi lililoleta fujo katika mkutano.
|
Jeshi la polisi likiwa limewakamata baadhi ya vijana ambao walikua wakileta vurugu katika mkutano wa ccm.
|
0 comments:
Post a Comment