Posted by Williammalecela.com on Friday, October 02, 2015
 |
| MWAPACHU - "Namuunga mkono Lowasa, lakini siwezi kuhama CCM kwenda CDM. CDM hawajitambui ila wamempata mwanaume." |
 |
| SOFIA SIMBA -" Nimefuatwa na vigogo wa CDM wakiniomba niungane nao kuleta
mabadiliko, nimewajibu mabadiliko ya kweli yataletwa na Magufuli na si
Lowasa. tulifanya makosa makubwa kutoka kikaoni, tuliona dalili za mtu
kuandaliwa.. tuliomba msamaha na maisha yanaendelea.. lakini
ninachofurahi ule mgomo wetu ulisaidia kuwafanya CCM kuchagua mgombea
mwenye sifa." |
 |
| MWANDOSYA - "Ni kweli nahama.. lakini nahama kutoka Dar kwenda kijijini
kwetu Lufilyo Busekelo.. ni kweli CCM walinikwaza lakini siwezi
kujidhalilisha kuhamia CDM chama ambacho siku zote nimehubiri kuwa ni
wababaishaji." |
NCHIMBI -
"Nimesoma hizo habari magazetini.. na nimefuatwa na viongozi wa
CDM kunibembeleza nihamie kwao.. hivi uanachama mtu anaombwa au
anaomba..maajabu ya Dunia ni kutoka chama mathubuti kama CCM na kuhamia Chama kinachoelekea kufa kama Chadema, habari za mimi kuhamia huko ni UZUSHI"
0 comments:
Post a Comment