Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Chamwino. Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ameapa kutotumia tena usafiri wa anga katika kampeni, baada ya helikopta aliyokuwa anatumia kupata hitilafu na kushindwa kuruka katika Kijiji cha Idifu wilayani hapa,
juziLusinde maarufu kwa jina la Kibajaji alithibitisha kuwa helikopta hiyo ilishindwa kuruka baada ya rubani kubaini ilikuwa na hitilafu, na ilikuwa imetua katika eneo la kichaka kijijini hapo.
Jana asubuhi alifika mtaalamu wa ndege kutoka Afrika Kusini na kuirusha hadi Dodoma Mjini.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
0 comments:
Post a Comment