Na Grace Shitundu, Dar es
salaam
MGOMBEA Ubunge jimbo la Kibamba kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Fenela Mukangara ametoa ahadi ya kupambana na kero ya maji
inayowakabili wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu.
Akizungumza katika mikutano ya Kampeni katika kata ya Msigani na Malamba mawili wiki iliyopita Dk. Mukangara amesema atashirikiana na wananchi kutatua kero hiyo kwa kuhakikisha yanapatikana mara tu atakapochaguliwa kuwa mbunge jimbo hilo jipya.
Alisema kuna sababu nyingi ambazo zinafanya jimbo hilo kuendelea kuwa na shida na maji hata hivyo zinaweza kutatuliwa endapo zitafatiliwa kwa ukaribu.
“Najua maji ndio kilio kikubwa cha watu wa jimbo hili ingawa kuna matatizo mengine yanayowakabili yakiwemo ya huduma za kijamii afya na elimu” alisema
Alisema moja ya sababu ya upungufu wa maji katika jimbo hilo ni baadhi ya wananchi wasio waaminifu kujiunganishia mitandao ya maji kiholela kwa ajili ya biashara.
Aidha aliongeza kuwa uchakavu wa mabomba kutoka mtambo mkubwa wa maji wa ruvu juu nao umechangia tatizo hilo ambalo amedhamiria kulitatua kwa nguvu.
Hata hivyo Dk. Mukangara amesisitiza kuwa na nguvu ya pamoja kutoka serikalini, wadau wa sekta ya maji na wafadhili kushirikiana kuchimba visima virefu na vifupi ili kukabiliana na kero hiyo.
Alitaja vipaumbele vyake vingene katika jimbo hilo kuwa ni pamoja na elimu, Afya, kuwawezesha wakinamama kwa kuanzisha na kuimarisha vikoba pamoja na ajira kwa Vijana.
Pia kutokana na jimbo hilo kuwa ni makazi mapya atahakikisha

0 comments:
Post a Comment