KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph
Makamba amemshangaa Kingunge Ngombale-Mwiru kutamka kwamba chama hicho
hakijafanya chochote wakati ndiye aliyeshiriki kuandika vitabu kadhaa vya
mipango ya chama hicho.
Katika hali ya kumsuta Kingunge aliyetangaza kuachana na CCM
hivi karibuni, Makamba alisema mwanasiasa huyo amekosa hofu ya Mungu kwa kusema
uongo dhidi ya chama hicho tawala.
Makamba alisema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni za
mgombea ubunge Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya CCM, Emmanuel Mwakasaka
uliofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mabasi cha Zamani mjini hapa.
“Kutokana na kukosa
hofu ya Mungu, kada huyo amekuwa akisema uongo na kufikia hatua ya kutaka
mabadiliko bila ya kutafakari kuwa yeye alishiriki kuandika vitabu
vinavyoelezea sera za chama hicho,” alisema.
Alitaja vitabu hivyo kuwa ni Mwongozo wa CCM cha mwaka 1971,
Mwongozo wa CCM cha mwaka 1981, Mwelekeo wa CCM katika miaka ya 1990 pamoja na
Mwelekeo wa CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010.
Katibu mkuu huyo mstaafu alisema kutokana na ushiriki wake
katika kuandika vitabu hivyo, mtu mwenye busara hawezi kusema kuwa CCM
haijafanya kitu katika kuwaletea maendeleo wananchi. Aidha alisema, kama hakuna mabadiliko Kingunge hawezi kukwepa lawama.
Alisema madai ya Kingunge kwamba CCM imekosa pumzi ni kauli
inayostahili kupuuzwa kwani aliingia kwenye chama hicho akiwa kijana na sasa
ameondoka akiwa mzee, hali inayoashiria kuwa hawezi kuendana na kasi ya
mabadiliko ndani ya chama.
Makamba alisema ameshangazwa kwa kitendo cha kada huyo wa
zamani wa CCM kumpigia debe mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa
wakati walishirikiana kumkataa Lowassa kwenye vikao vya Halmashauri Kuu ya
Taifa kwa madai kuwa ni fisadi, hastahili kuwa kiongozi wa nchi

0 comments:
Post a Comment