Tuesday, October 27, 2015



Mawaziri watano wa Serikali inayomaliza muda wake, Mawaziri wawili wa zamani pamoja na wagombea wengine maarufu wa Bunge lililopita Wataungana nasi kulifuatlia Bunge la 11 kupitia Luninga.


Mawaziri Steven Wasira (Waziri wa Kilimo na Chakula), Christopher Chiza (Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwezeshaji na Uwekezaji), Mhe Aggrey Mwanri (Naibu Waziri wa Tamisemi), Dk Steven Kebwe , (Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii)
 

na Anne Kilango Malecela (Naibu Waziri wa Elimu) Wamepoteza IMANI kwa Wapiga kura wao Sawa Pia kwa Mawaziri wa zamani wawili, Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Balozi Khamis Kagasheki na Omary Nundu (Uchukuzi) kwa mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa.
 

Somba Somba hiyo pia Imewakumba Wabunge maarufu kama Vincent Nyerere (Musoma Mjini), James Lembeli (Kahama Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Ezekieah Wenje (Nyamagana), Kyisieri Chambiri (Babati Mjini).
 

Pia aliekuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mikoa wa CCM, Mgana Msindai ambae alihama CCM ili Kumfuata Lowassa Ukawa nae pia Ameambulia Patupu kama ilivyokuwa kwa "Shemeji" Henry Kilewo ambae ni Mume wa Mwanaharakati Joyce Kiria wa ‪#‎WanawakeLiveTvShow‬ ambae alichapwa na Mkongwe Prof Jumanne Maghembe.

0 comments:

Post a Comment