JUU: Mwanadada anayekuja juu katika filamu Bongo, Tiko Hassan. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Tiko alisema baada ya uchaguzi, wasanii wa filamu wana kazi nzito ya kuirudisha tasnia yao ambayo imefifia kutokana na wengi kujikita kwenye kampeni wakisahau kazi yao.
“Wanasingizia hakuna soko, lakini hilo siyo tatizo, tatizo ni sisi wasanii kwa sababu hatujui nini tunachotaka hivyo tunatakiwa kubadilika na kujua ni kitu gani tunataka, sanaa imekufa, tuna kazi nzito sana ya kuifufua ili irudi kama zamani,” alisema Tiko.
0 comments:
Post a Comment