Posted by Williammalecela.com on Sunday, October 11, 2015
 |
| Ninaamini hakuna binadam aliyeumbwa kuwa Neutral, soma hili gazeti chini halifichi kwamba lipo 100% on Chadema na UKAWA side, sijawahi kumtukana mtu wala kumuamulia binadam yoyote kukubali mawazo yangu mimi huwa ninaweka facts uamue mwenyewe. Ninapenda CCM na ni mwanachama wa CCM na Chama changu ninakihitaji sana hasa now kuliko kinavyonihitaji kutokana na Usanii wa ajabu ambao nimeuona na ninauona kwa macho yangu wa wananchi kdanganywa kama watoto wadogo na wajanja wachache ambao hawana nia njema na Taifa zaidi ya kupigania madaraka na uroho wa mali za umma. Kwa mfano 1. Lowassa leo anatuaambia kwamba atamrudisha Balali kwa sababu anajua alipo, huu ni uongo na ujinga sana binafsi naijua familia ya mke wa Balali, I grew up with them nilienda kwenye msiba ninamjua mke wake kwa karibu sana ni mtoto wa Mmoja wa wachungaji wa kwanza wa Kilutheri Tanzania mpaka ni Walutheri leo, najua kwamba Mwili wa Marehemu Balali ulikuwa cremated kule DC Washington, baadaye Mke na watoto wake wakarudi na Majivu Iringa ambako sala zote za Msiba zilifanyika. Leo mgombea Urais ananiambia kwamba wote ule ulikuwa ni uongo na yeye alikuwa Waziri Mkuu now kwa nini hakusema then kwamba wananchi wandanganywa Balali hajafa? nasema ni mambo kama haya ndio yananifanya nipigane usiku na mchana kuwaokoa wananchi na Taifa langu na hawa wahuni waroho wa madaraka. 2. Lowassaa anasema atamtoa Babu Seya gerezani maana kifungo chake ni cha kuonewa na kuna wajinga wanamuamini cause hawajui kwamba kuna watoto 9 waliolawitiwa na huyu Mzaire na mtoto wake, Ushahidi upo na ulionyeshwa mahakamani watoto wapo mashahidi pamoja na Mwalimu aliyekuwa anawapeleka hao watoto kwa Babu Seya yupo, ninachukizwa na uongo wa makusudi wa Lowassa kwenye kutafuta kwake madaraka. I can go on and on like Kweli ninataka kuongozwa na Rais anyeshauriwa na Askofu kama GWajima? hapana ndio maana ninapigana kwa kutumia kila kitu nilichonacho kuipigia debe CCM kama kuna mwenye tatizo anisubiri uchaguzi uishe kwanza then rudi hapa kuendelea na habari za kawaida kama zamani ila kwa sasa na huu uchaguzi, please utasubiri sana cause ninafuata nyayo za gazeti la Tanzania Daima tu!! - Le Mutuz Nation |
 |
|

0 comments:
Post a Comment