Wednesday, October 7, 2015

Bwana Yesu asifiwe.
Tarehe kama ya leo, Oktoba 07, 2014, tulimpoteza baba yetu mpendwa, Mzee Christopher Salimu Kisaka, alipofariki katika Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam. Ni mwaka mmoja sasa umetimia tangu uiage dunia, lakini kwetu sisi uliyotuacha tunaona kifo chako ni kama vile kimetokea jana tu. Maumivu tunayoyapata kutokana na pengo uliloliacha ni makubwa na makali sana yasiyoelezeka kwa urahisi. Faraja na imani tuliyo hivi sasa ni kwamba umekwenda kupumzika mbele ya Kiti cha Ufalme wa Mungu. Raha ya Milele umjalie ewe Bwana na Nuru ya Daima umwaangazie. Astarehe kwa amani. AMEN

0 comments:

Post a Comment