Posted by Williammalecela.com on Wednesday, October 14, 2015
 |
| Mapokezi makubwa sana yanamsubiri Super Star Diamond Platznumz atakaporejea nyumbani kesho Alhsamis mchana akitokea Marekani ambako alishinda Tunzo zingine 3 kubwa za Africa kwa mpigo. Mapokezi hayo yanatazamia kuanzia Uwanja wa Ndege, kupitia Kariakoo baadaye yataelekea Tandale alikozaliwa Mwanamuziki huyu maarufu sana sasa hivi Afrika Mashariki nzima na Duniani. Na mwisho wa Mapokezi haya itakuwa ni ukumbi wa starehe wa Escape One Beach, ulioko Mikochen ufukweni mwa bahari na wasimamizi wa Mapokezi hayo wamesema hakutakuwa na kiingilio ukumbini hapo. |
0 comments:
Post a Comment