BASI
tena! Kifo cha ajali ya gari cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia (DP) na Kiongozi wa Kanisa la Full Salvation, Mchungaji
Christopher Mtikila kimewaacha wananchi na majonzi makubwa lakini nyuma
yake, Uwazi limebaini maswali 10 tata kuhusu ajali hiyo.
Ajali hiyo
ilitokea saa kumi na mbili asubuhi ya Jumapili iliyopita, eneo la
Msolwa, Chalinze wilayani Bagamoyo, Pwani ambapo gari aina ya Toyota
Corolla lenye namba za usajili T 189 AGM lilipoteza mwelekeo na kuingia
bondeni. Mtikila alipoteza maisha papohapo huku watu watatu, akiwemo
dereva wa gari hilo wakinusurika.

0 comments:
Post a Comment