Posted by Williammalecela.com on Thursday, October 15, 2015
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Jangwani Moddy Bawaziri akiwa na Mke wake Bi Mariam Bawaziri wakiwa na watoto wao 3 wa kwanza kushoto Salim, kulia Omar na wa mwisho kati kati Omar wakiwasili kwenye Ukumbi wa Shekinah Gadern Mbezi Makongo tayari kwa ajili ya Sherehe ya kutimiza miaka 14 ya ndoa yao. Bawaziri ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Michezo nchini na pia ni Mjumbe wa Kamati ya Miss Tanzania, amekuwa akijihusisha sana na kunyanyua mchezo wa Ngumi za kulipwa. Akizungumza kwenye hafla hiyo Bawaziri alisema ana bahati kupata Mwanamke mvumilivu na mwenye upendo na huruma kama mkewe Bi Mariam. Sherehe hizo zilizofanyika huko Mbezi Makongo zilihudhuriwa na watu wengi maarufu hapa mjini Dar.
Wajumbe wa zamani wa Kamati ya Miss Tanzania wakiongozwa na Uncle Lundenga, Bosco Majaliwa, na Albert Makoye ni baadhi ya watu maarufu waliokuwepo kwenye sherehe hizo pia The King Of All Bongo Social Media Le Mutuz Nation alikuwepo.
Wageni waalikwa from Nkurumah Team walikuwepo pia.
Mwenyekiti Moddy Bawaziri akizungumza na Wageni waalikwa.
0 comments:
Post a Comment