Monday, October 5, 2015





"Tarehe 30 Septemba 2015 niliandika katika ukurasa wangu wa fb makala fupi sana nikijibu swali nililoulizwa na watu wengi kuhusu mimi kuhama Chama. Majibu yangu naamini yalieleweka. Siku mbili baada ya hapo wataalam wa propaganda wakaongeza maneno yafuatayo kwenye taarifa ya majibu yangu....." ni kweli CCM walinikwaza lakini siwezi kujidhalilisha kuhamia CDM chama ambacho siku zote nimehubiri kuwa ni wababaishaji".

Maneno haya yaliyoongezwa sio ya kwangu na wala hayaendani na staili yangu ya uandishi. Kuhariri taarifa ya mwandishi na kuongeza maneno yasiyo na uhalisia na taarifa hiyo na kuisambaza bila mwandishi kujua, ni aina ya dharau na si uungwana".-Prof. Mark James Mwandosya

Pia siku chache baada ya waziri wa nchi ofisi ya rais kazi maalum Professa Mark Mwandosya kudaiwa katika mitandao ya kijamii kuwa anahamia ukawa amesema suala la kuhama chama ni la mtu binafsi kwakuwa serikali ni endelevu yeyote anaweza kuingia madarakani bila kujali chama na kwamba vyama vya upinzani ndivyo vinavyoifanya serikali yeyote ile kufanya kazi kwa umakini katika kutumiki wananchi wake.

0 comments:

Post a Comment