Thursday, October 22, 2015

Shaka.  afichua mpango  hatari wa chadema kuihadaa dunia
Na Mwandishi  etu ,Dar  es  salaam 
Katibu mkuu  wa umoja wa vijana wa ccm  (uvccm) Shaka Hamdu Shaka amesema uvccm imebaini mpango hatari unaoandakiwa na upinzani  kumteka nyara mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa ili ionekane kuna njama za kumhujumu mgombea  huyo kabla ya uchaguzi oktoba 25 mwaka huu. 

 Amesema mpango na mkakati huo unalenga pia kuipaka matope Tanzanai ionekane mbele ya jumuiya ya kimataifa haiheshimu misingi ya demokrasia na inamhofia mgonbea huyo. 


Shaka alisema hayo katika viwanja vya Biafra wilaya ya Kinondoni mkoani dar es salaam .

 Alisema vile vile  kuna njama na mkakati wa chadema kuwa alishaona vijana wake nguo za ccm hatimae  kuchoma gari anayotumia lowassa ili kuiaminisha dunia  anahujumiwa na serikali ya chama tawala na haiko tayari kwa matokeo .

 "Nataka niwape tahadhari na indahar vijana wenzangu dhidi ya mpango hatari unaosukwa na chadema , wanajiandaa kumteka nyara Lowassa na kumficha ionekane amehujumiwa na ccm kabla ya oktoba mwaka 25  "alisema  Shaka 

Alisema chama hicho na mgombea wake anayeungwa mkono na ukawa katika kutapatapa kwake baada ya kuona hesabu zao za kuweza  kushinda zikikataa na kuwapiga chenga ,pia  wamewaandaa vijana wa chama hicho wavae sare za ccm , kupiga watu , kuvunja magari mitaani na kuipakazia mbele ya dunia . 

 Shaka aliitaka jumuiya ya kimataifa,nchi wahisani, mashirika ya kiraia ya ndani na nje, waangalizi wa nje na ndani kuelewa mpango huo wa chadema na ikiwa hilo litatolea si uvccm na vijana wake wanaohusika na jambo hilo. 

 "Tunaitangaziabdujia kwa sauti ya juu dunia ya wapenda haki, usawa. , haki na demokrasia kubaini mpango huo. , serikaki ya ccm kwa miaka zaidi ya 50 imekuwa ikiheshimu, kuenzi na kufuata misingi ya demokrasia , utawalabora na kutunza msingi amani na utulivu.

 Katibu mkuu huyo wa uvccm alisisitiza kuwa anaamini serikali ya ccm kama mhimili wa uswa na tegemeo la ukombozi kusini mwa Afrika. ,kamwe  hakitahusika na uvurugaji wa amani wala kudhihaki miiko ya demokrasia. 

 Hata hivyo aliwataka vijana waliojiandiiisba katika daftari la kudumu la wapiga kura kuitokeza mapema ili kupiga kura na kurejea majumbani na kusubiri matakeo yatakayotangazwa na chombo halali chenye dhamana ya kisheria  Tume ya Taifa ya uchaguzi  (NEC). 

 "Nawaasa tena na tena vijana wenzangu Tannzania Bara na zanzibar kujiepusha na vitendo vya uvunjaji amani kwa kuchochewa na viongozi wa kisiasa ambao wao na  watoto  wao hawatakuwa sehemu ya maandaamano wala  vurugu hizo" alisema shaka l 

0 comments:

Post a Comment