MCHUNGAJI wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima sasa amejipapambunua hadharani msimamo wake, jambo ambalo ni tofauti
kabisa na viongozi wengine wote wa Dini nchini akiwa sanjari na swahiba wake
Edward Lowassa anayempa mbinu za kufufua mizimu,
ili wapate wafuasi.
Viongozi ni binadamu na wanastahili kuwa na utashi
wa kisiasa, lakini hili la mmiliki wa Kanisa kusimama kiongozi wake kwa swahiba
wake Edward Ngoyai Lowassa, ndiko ambako awali watathamini wa siasa nchini
walisema, tatizo si Lowassa peke yake na genge lililowazunguka nalo kama
likiingia IKULU ni tatizo ambalo heri mara 100 ya CCM ya sasa.
Lowassa ambaye CHADEMA badala ya kumfanyia kampeni kwa
wakati huu wanamhangaikia kumsafisha, huku wanaomzunguka nao wakiwa wachafu mikononi,
usoni na mioyoni mwao. Wana sifa nyingi zenye mushkeli kwa afya ya mustakabali
wa amani,upendo na pasipo na chuki wala IKULU kuvamiwa na genge la walanguzi
walio midomo wazi wakiisubiria kama Mafisi.
Gwajima swahiba wa Lowassa aliwahi kuutangazia umma
wa Watanzania kuwa anataka kumfufua kada na mbunge wa viti maalum CCM, marehemu
Amina Chifupa aliyekuwa mke wa marehemu Meddy Mpakanjia ‘CK’.
Gwajima mwenye kushabihiana mambo mengi na mgombea
wa CHADEMA Lowassa kikauli na mitazamo, pia alipata kutoa kauli nyingine ngumu
ambazo nazo hadi sasa hazijatekelezwa ikiwemo ya kutaka kumfufua aliyewahi kuwa
Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine.
Kushabihiana kwao, kiahadi zao na aina ya matendo ya
kusema maneno magumu kwa mgombea wa CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa ambaye nae naye
amewaahidi Watanzania kuwaletea aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, marehemu
Daud Balali.
Ufufuo wa Lowassa unatofauti gani na ndoto za mchana
za Gwajima ambaye alipata kufikishwa mahakamani kwa tabia na kauli zake kuwa atafufua
misukule? maana yake ni kutaka kupata wafuasi wengi kanisani kwake ambao
kimsingi wana matarajio tofauti na mmiliki wao.
Lowassa maana yake anataka kumsuta mhariri mtendaji
wa gazeti la Tanzania Daima, Nevil Meena gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe. Bwana Meena ni katibu wa jukwaa la wahariri ni mtu makini
sana, mwenye kuiheshimu taaluma yake, sijui atapotoka vipi leo akituaminisha
kuwa habari alizotuhuthibitishia Watanzania kuwa Balali alikufa, si kweli yu
hai.
Akiwa mhariri wa Mwananchi Jumapili wakati huo,
Meena alikwenda kuihoji familia ya Balali nchini Marekani na kupiga picha ya
kaburi la marehemu Balali. Katika habari ile aliwahoji mke, dada na watu wa
karibu kabisa wa familia hiyo, waliothibitisha kifo cha ndugu yao na kuwa
alizikiwa nchini Marekani, inawezekanaje leo aseme habari ile ni uongo, ukweli
ni anaosema Lowassa.
Tuache siasa, tusitake kwenda IKULU kwa uongo wa
kupata wafuasi. Mbali ya gazeti la Mwananchi, pia gazeti la Mtanzania
liliandika habari hiyo ikiwemo na uthibitisho wa familia iliyopo kijijini kwao
na waliopo nchini Marekani. Meena alikwenda Marekani ambako ni zaidi ya masaa 15
kutoka Tanzania kwa usafiri wa Ndege kwenda kusaka ukweli na kuondoa minong’ono
iliyokuwa imetanda kuwa Balali yu hai.
Si haki hata chembe kuitumia familia ya marehemu Balali
kuingilia IKULU, walipata msiba mzito sana, waliumia sana, lakini kwa kuwa ni
kazi ya Mungu, walishukuru na kumuombea astarehe kwa amani, leo hii mnawatangazia
ataletwa Tanzania, nini maana yake? Akitokea wapi? Lowassa nawe ni mzee wa ufufuo?
Gwajima si mtu safi, hata kidogo ukimsikiliza Dk.
Willbroad Slaa katika hotuba zake zote, hata siku moja hakupata kuzungumzia
mahusiano ya kifamilia, si kwa Freeman Mbowe, Tundu Lissu wala kwa Gwajima
mwenyewe ambaye hajajisafisha hadharani madai ya kuzaa na mwimbaji wa nyimbo za
Injili, Frola Mbasha, ambaye ni mke wa mtu.
Leo hii waliokuwa wakimtetea Gwajima kwa sakata lile
la kumpora Emmanuel Mbasha mkewe, hata kama wanampenda vipi mchungaji huyu, ni
wazi usafi wake umeingia matundu kiasi si rahisi waamini vinginevyo kutokana na
maneno yake na matendo yake ya sasa.
Lowassa amewaahidi Watanzania kuwa atamtoa Nguza
Viking na Pappii Kocha, je katika utafiti wake kuwa vifungo vyao vinatia shaka
amewauliza walimu wa shule ya msingi Mapambano pale Sinza? Amewauliza majirani
wa Sinza kijiweni? Atapata aibu maana wazazi walioathirika na jambo lile, mioyo
yao itapata kutu kumsikiliza binadam huyu asiye na huruma kwa malaika wale
waliodhalilishwa.
Jaji Thomas Mihayo aliyekazia hukumu ya maisha kwa
Babu Seya ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Baraza la Habari Nchini, ni mtu
mwenye kuaminika sana katika jamii, ana heshma kubwa sana jaji huyu mstaafu leo
hii ukimwambia hukumu yake aliitoa kwa maelekezo sidhani kama Jaji yeyote
nchini anayemjua na walimsifia sana wakati akistaafu kwa hukumu ile, majaji wa
Tanzania watakuelewa?
Ni kujenga chuki ndani ya jamii yetu ni kuondoa
dhana ya utawala bora. Gwajima mshenga wa Lowassa kuingia CHADEMA, ni maswahiba
wa kauli zao ngumu, ahadi zao zenye kukinzana na Mwenyezi Mungu, wanaweza
mshambulia mtu yeyote ilimradi waende IKULU, aah mzee wa maharage ya wapi!
mjinga mmoja, asiyefaa mmoja !.
Hakukosea kuwa mshenga wa mzee wa maamuzi magumu
mwenye uwezo pia wa kufufua watu ambaye pia mwenye kutaka ushindi wake utokane
na waumini wa dhehebu lake, loh kama mwalimu angekuwepo leo angetoka hadharani
na sijui angetamka nini dhidi ya Watanzania hawa wawili.
Hatahivyo, Hongereni kwa urafiki wenu. Watanzania
tuwe makini sana tunaofikiria kuwapa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Le Mutuz Nation - The King Of All Bongo Social Media.
|
0 comments:
Post a Comment