Friday, October 2, 2015


¤Mwaka huu hakuna uwezekano wowote wa kuwepo kwa BAO LA MKONO. Au lolote lenye kufafana na lile Diego Maradona aliloifungia Argentina dhidi ya England kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1986 lililofanyika nchini Mexico.


¤Tume ya Uchaguzi imekubali matokeo ya urais kutangazwa na kubandikwa kwenye vituo papo hapo kama ilivyo kwa udiwani na ubunge na si makao makuu kama ilivyozoeleka.

¤Kwa hiyo mtu yoyote anaweza kujumlisha hata kwenye Microsoft Excel na kupata matokeo.

¤Tume pia imepiga marufuku utaratibu wa kusafirisha masanduku ya kura kwenda kuhesabiwa wilayani au kwenye manispaa.

¤Kisheria NEC inatakiwa itangaze matokeo ya mgombea urais ndani ya siku 7. Lakini wameahidi kutangaza ndani ya siku 3 au 4 ili kukwepa uchakachuaji.

¤Pia katiba ya nchi ibara ya 74(11) inasema "katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yoyote au ya idara yoyote ya serikali au maoni ya chama chochote cha siasa".

¤Bila shaka mwaka huu hakutakuwa na malalamiko yoyote ya bao la mkono au uchakachuaji wa matokeo.

¤Mwaka huu hakutakuwa na sababu yoyote ya maandamano ya nchi nzima yasiyo na ukomo au ususiaji hotuba za rais za ufunguzi wa bunge.

¤Nimeona baadhi ya vyama vikitaka washabiki wao wasiende mbali ya vituo baada ya kupiga kura. Sijaona umuhimu wa hili kama vyama vina mawakala wanaowaamini.

¤Pia nimeona kuna msisitizo wa vyama kupewa mapema daftari la kudumu la wapiga kura (soft copy).

¤Mpaka sasa sijajua hata mtu akipewa daftari la wapiga kura litamsaidia nini.

¤Uchachuaji upo kwenye kuhesabu pamoja na kubadili matokeo siku ya uchaguzi.

¤Japokuwa usajili wa voters ni electronic, lakini upigaji kura bado ni manual. Mtu mmoja hawezi kupiga kura mbili maana wino wa kidole utakuwa haujafutika na mawakala wa vyama wataona.


  • Comments
    • Bob Ramso
      Bob Ramso Ahsante...Wanasiasa Waache Propaganda za Kuwajaza Watu Matumaini Mwisho wa Siku Kura ni Siri Muhimu ni kuwatangazia Sera Ili Wananchi Wazielewe na Hatimaye Wajitokeze Kupiga Kura Sio Kushindana Nani Kajaza Watu au Yupi Kakodi Watu..
      Like · Reply · 1 · 23 mins
    • Bonaventura Kasema
      Bonaventura Kasema Bado hatuko sure na software itayofanya tallying tunataka tuione kama haina sub programme ya kuduplicate tallying by a certain factor
    • Marwa Mwita
      Marwa Mwita Asante William Kaijage lakini
      1. Mimi naona bado ni muhimu kutoa daftari ya wapiga kura (softcopy) mapema kama reference wakati wa majumuhisho ya kura...

      2. Wino wa kidole sio wa kuuamini 100% kwamba haufutiki...lakini ni vizuri kuwa na njia nyingine makini zaidi ya kuchovya wino kwenye kidole..ili watu wasipige kula zaidi ya mara moja...
    • Bonaventura Kasema
      Bonaventura Kasema Nec hatuwez waamin sana kwan si huru ni kitengo cha serikali mkuu wake no mteuliwa wa rais ambae chama chake kiko hati hati kutolewa je atakubal kirahis? Inabid watu convince sana kuhusu how transparent they are sio kauli za mdomon

0 comments:

Post a Comment