Nimesikitishwa
sana na orodha ndefu ya vijana wanaoshikiliwa na wengine wameshatolewa
hukumu ya kunyogwa wengi wao ni kutoka Tanzania, lakini hii inatokana na
vijana wengi wa kitanzania kudanganywa kwa kutaka utajiri wa haraka
haraka.
Usijaribu
wala usidanganywe kupeleka madawa ya kulevya hasa katika miji ya Macao,
Hongkong,Indonesia, maana ni hatari sana kwani kifungo cha chini kabisa
kwa gram moja ni 7 years,ila wengi uhukumiwa kwa kunyogwa na kifungo
cha maisha na kazi ngumu.
Matajiri wengi uwadanganya vijana matokeo yake uishia magerezani na kunyongwa.
Jana
Indonesia imewapiga risasi raia wa nchi tano zikiwemo zenye nguvu
kiuchumi kwa raia wake kuingiza madawa ya kulevya nchini humo,licha ya
nchi hizo kuwaita nyumbani mabalozi wake.
Jamani
usidanganywe heti utafungwa miaka 2 utatoka, matajiri waelezeni ukweli
kabla ya kuwatuma huko, mimi nilikuwa mji wa Macau ukweli hali
inasikitisha kwa watanzania wanateseka sana.
0 comments:
Post a Comment