
Familia ya Mgombea Urais wa UKAWA Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa, ikiongozwa na Fred wawepo vituoni kulinda kura zao na za baba yao.
Bi Awena Sinani Masoud na mwanaye wa Kike, wawepo Vituoni mwao walinde kura zao na za baba wa familia yao.

Kijana wa Miaka 22, Clinton Freeman Mbowe (kushoto) itapendeza kama ataongoza kundi la walinda kura kituoni kwake.
Najua jambo hili litaibua fikra kama zangu katika baadhi ya vichwa vya wanajamvi humu ndani lakini pia najua nimealika mvua ya matusi na maneno ya shombo kutoka kwa wale jamaa zangu wa "kazi maalumu" wa kule ngome, mtaa wa maguruwe - Mbezi na wale wa pale kituoni Ufipa. Lakini vyovyote iwavyo sitaacha kufikiri na kushirikisha wenzangu katika fikra zangu.
Wanaposema tukalinde kura, nafahamu kuwa wanamaanisha hawa hapa chini kuwa ndio walinzi wa kura zao..

Kwa ulinzi wa ndugu zangu hawa, sidhani kama "salama" itapatikana. Ila vyovyote iwavyo nawatakia kila la heri kwa "mpango huu" Kwa muda sasa kumekuwa na mjadala wa kile kinachoitwa "KULINDA KURA" na kwa kuwa muda mwingi niliutumia vijiji vya Mbeya nikifanya kazi tukufu ya kuwahubiria neno la kweli wananchi wa nchi hii iliyobarikiwa ya Tanzania kuwa mabadiliko ya kweli yapo ndani ya CCM na kwamba wamkatae shetani na wafuasi wake kwa kukataa wala rushwa na mafisadi wa nchi hii, walioliangamiza Taifa hili kwa miaka mingi kwa uroho na ubinafsi wao.
Kwa kuwa sasa "kazi hiyo takatifu" imeshatimia, na wanambeya wamenielewa, sina tena shaka na maamuzi yao ifikapo October 25, hivyo nimepata fursa ya kurudi tena kujumuika na wanajamvi wengine kujadili hoja na vioja mbalimbali vinavyoletwa hapa Jamvini kila uchao.
Kwa mtazamo wangu, sioni tatizo kabisa kwa watu kulinda kura zao, hata ikiwa watu hao wanataka kukaa sentimeta moja kutoka ilipo kura hiyo, nasema hivi nikiamini kuwa kura ni mali kama zilivyo mali nyingine hivyo ulinzi wake ni jambo la msingi sana.
Na nawaunga mkono Viongozi wa Upinzani wale "wanaoshadidia kuwa kura zao lazima zilindwe" na wanasisitiza kuwa hawamuamini yeyote hata wasimamizi wa kimataifa..nasema ni sawa tu ikiwa tutawaona wao wakiwa mstari wa mbele kulinda kura hizo kama walivyo mstari wa mbele kuhimiza Ulinzi huo.
Ila matukio na taarifa (ambazo baadhi nimeshazithibitisha na nyingine bado ni tetesi) zimenipa mashaka juu ya dhamira halisi ya hiki kinachoitwa KULINDA KURA.
1. Taarifa za kuhamishwa kwa mabilioni ya fedha kutoka kwa Viongozi wakuu wa UKAWA, wahisani na wadau zimenistua kidogo, nikijiuliza kwanini mabilioni hayo yahamishwe sasa..??? kwanini yanakimbizwa nchini..? Napata mashaka kuwa watu hao wanajiandaa kuanzisha makazi mapya na maisha mapya kule ambako zimehamishiwa fedha hizo.
2. Taarifa za safari za familia za Vigogo hao wa UKAWA nazo zinatia mashaka, taarifa za safari ya Mke wa Maalim Seif Sharrif Bi Awena Sinani Masoud pamoja na mtoto wake wa kike kuondoka nchini tarehe 16 Oct 2015 zinaukakasi, kwanini waondoke wakati huu, vipi kuhusu haki yao ya kupiga kura..? Vipi kuhusu himizo la kulinda kura..? Ama wao sio wahusika ama walengwa wa mpango huo..?
3. Safari ya Franklin Frederick Sumaye kwenda Hosuton, Texas nchini marekani hivi karibuni, inanifanya kuhoji uelewa wa umuhimu wa "kura" kwa Viongozi wa UKAWA hata waruhusu watu walio na uhakika kuwa watawachagua waondoke katika kipindi hiki, ina maana hawazihitaji kura zao, ama hawaitaji ulinzi wao..?
Mimi nasema na kuendelea kusisitiza kuwa suala la Kulinda kura ni "HAKI" ya kimsingi kabisa ya yeyote yule, hivyo CCM wanayo haki hiyo na vyama vingine pia..lakini wale wanaohimiza jambo hili tunataka kuwaona wakilinda kura hizo pamoja nasi, tuzione familia zao zikilinda kura zao..sio sisi kajamba nani..!!
Nataka wafuatao wawe vinara wa kulinda kura katika vituo walivyojiandikisha, ili na sisi wengine tukalinde zetu katika Vituo vyetu..namaanisha hawa wafuatao kwenye picha hizi;
0 comments:
Post a Comment