Muimbaji huyo alikuwa ametajwa kuwania vipengele vinne kwenye tuzo za Afrima zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria.
Kiba
alitajwa kuwania Best Male Artist East Africa, Artist of The Year, Song
of the Year na Song Writer Of The Year In Africa. Tuzo tatu kati ya
hizi zimechukuliwa na Diamond waliyekuwa wametajwa pamoja.
Kupitia post aliyoweka kwenye Instagram, Alikiba amedai kuwa anaamini ‘kuna watu’ wanaotumia fedha kuhakikisha anakosa tuzo.
“Asanteni
sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya
kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza
pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will
always be there for you #hapakazitu #kingkiba,” ameandika Alikiba.
Kauli yake imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa muziki.

0 comments:
Post a Comment