Tuesday, November 3, 2015

Mashabiki wa Alikiba na Christian Bella muda si mrefu watapata kusikia
na kuona collabo ya wakali hao waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu kwa muda
mrefu.

Bella na Ali Kiba


Kiba na Bella ambao wameshoot video ya wimbo wao mpya ‘Nagharamia’
nchini Afrika Kusini, wamesema kuwa wimbo huo una story nzuri ambayo
inaweza hata kutengenezewa filamu.

“Nyimbo tuliyoimba inaweza ikawa hata sound track ya movie kwasababu ni
story ambayo inavutia, inapendeza…” Alikiba alifunguka kupitia 255 ya
XXL. “Ni idea nzuri ambayo inahitaji hata kufanyiwa movie ikipata nafasi
vile vile uwezekano huo wa kufanya upo.”

Kiba na Bella wametoa dili kwa yeyote ambaye angependa kutumia idea ya
wimbo wao kufanya nao movie, kuwa wako tayari endapo watawekewa mezani
shilingi milioni 700.

“Akija na mtonyo akiweka mtonyo tutafanya tu” alisema Bella. “Kwa haraka
haraka labda milioni 700 hivi” aliongezea Kiba.

King Kiba ameongeza kuwa tayari wamesajili wazo lao, hivyo bila kiasi
hicho cha pesa mtu yeyote hataruhusiwa kuitumia.

Wimbo pamoja na video ya ‘Nagharamia’ vitatoka kwa pamoja mwezi huu wa
Novemba.

0 comments:

Post a Comment