Posted by Williammalecela.com on Tuesday, November 17, 2015
Yanayojiri Bungeni leo Novemba 17, 2015 - Uchaguzi na kiapo cha Spika wa Bunge la 11
Karibuni hapa katika kujulishana mambo yanayojiri katika Kikao cha
Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania leo hii Mjini Dodoma. Niko hapa na nitajitahidi kuwapatieni
updates kwa kadiri ya uwezo wangu. Naamini Mods pia watakuwa
wakinisaidia kwani sometimes ndani ya ukumbi wa bunge network huwa ya
kusuasua. Hata hivyo nipo imara kuwajulisheni.
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano linaanza leo Dodoma kwa kusomwa
Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge, uchaguzi na Kiapo cha Spika, Kiapo
kwa wabunge wote
Muda huu tayari wabunge wameanza kuwasili kwenye viwanja vya Bunge na
wengi wamo kantini hapa wakipata staftahi kabla ya kuingia rasmi
ukumbini.
Update.
Wabunge wengi wanaingia bungeni now harakaharaka maana mida wowote Kikao
kitaanza. Changamoto iliyopo ni kuwa.baadhi ya wabunge hasa wapya
wamevaa mavazi ambayo sio ya kibunge jambo ambalo ni kinyume na kanuni.
Labda ugeni utawaokoa wasitolewe nje
Updates
Katibu wa Bunge Dr Kashililah ndio anaanza kwa kusoma tangazo la Rais
kuitisha bunge la 11. Mkutano wa uchaguzi unaanza na Andrew chenge
anateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda kuongoza uchaguzi wa spika. Chenge
kaingia na uchaguzi unaanza kwa wagombea kuitwa kujieleza
Updates
Wagombea wote wameruhusiwa kuingia ndani na wameingia ukumbini isipokuwa
Hashim Runngwe ingawa hajajitoa hivyo anaruhusiwa kupigiwa kura bado
Updates
Wagombea wametoka nje na wanaitwa mmojammoja kujieleza kwa dakika tatu na maswali matatu kama yapo
==============
Wanaogombania nafasi ya uspika wanaendelea kuomba kura na
sasa ni zamu ya aliyekuwa naibu spika wa bunge la kumi, Job Ndugai.
Amesema anaelimu ya kutosha na uzoefu pia yeye ni mbunge mwenzao hivyo
anaekaa na mgonjwa ndiye anayejua matatizo ya mgonjwa.
Selasini(Swali): Ni namna gani kama spika utasimamia vyombo mbalimbali vya bunge?
Ndugai: Niwahakikishie taasisi ya bunge naifahamu vizuri ikiwemo vyombo na kamati zake, kwa uzoefu na elimu msiwe na wasiwasi.
Tizeba(Swali): Ndugai! Tukiacha mambo ya utani kati yangu na
wewe, ningependa kujua uzoefu unaousema mbona haufanani na umri wako,
ningependa kujua umri wako kama hutojali.
Chenge: Hilo sio swali.
Kunchela(Viti maalum Katavi): Kwa tathmini ya bunge lililopita ulionesha ubabe, umejipangaje kuendeleza ubabe huo ukipata nafasi?
Chenge: Hilo sio swali, ni maoni yako.
Wabunge wanaomba utaratibu na Chenge anagoma.
Molell: Baadhi ya wabunge walitoka nje bunge lililopita, Ni kwa namna gani atahakikisha bunge hili
Zitto(Utaratibu): Bunge likishaisha na mambo yake yanaisha, toka
maswali yanaanza mwenyekiti umekuwa unaruhusu maswali kwa reference ya
mabunge yaliyopita.
Chenge: Silichukui hilo la Zitto Kabwe na Ndugai jibu hilo kwa kifupi
Ndugai: Nawahakikishia bunge la amani, umoja na upendo, nawaomba kura zenu, hapa kazi tu.
Anaefuata sasa ni Ole Medeye kupitia CHADEMA
Medeye: Sheria zinazotungwa na bunge hili ndio msingi wa kugawa
haki katika bunge hili, lengo langu la kwanza nitakalolisimamia ni
kuhakikisha tunapata katiba mpya. Jambo la pili natambua wa bunge katika
kuisimamia serikali, nitaomba kama bunge tufanye marekebisho
makubwa.(Muda umeisha) Nawaomba kura zenu ili tuweze kufanya marekebisho
hivyo wabunge mnipe fursa, naomba kura.
Bobari(Mchinga): Natambua mgombea ni mzoefu serikalini, unadhani kasi ya bunge hili inahitaji spika wa aina gani kuendana na kasi hii.
Medeye: Wabunge walio wengi ni vijana hivyo mtazamo wa bunge hili
ni kesho na sio jana, nikipewa fursa hiyo nina uwezo wa kusimamia bunge
hili, dhima yangu mojawapo ni kurekebisha bunge.
Nape: Nakushukuru, naitwa Nape mbunge wa Mtama. Kumbukumbu
zinaonyesha ulishawahi kutolewa na ndugu Lema una tuhuma za ubaguzi,
sijui tabia hizo umeshaacha!
Chenge: Hilo sio swali
Jaffo: Watanzania wamekubali slogan ya Magufuli ya hapa kazi tu, mbunge amejipanga vipi kuhakikisha tunaenda na kasi.
Medeye: 2010 nilinadi ya ari zaidi lakini hatukuenda na kasi hio, tunachotaka ni serikali kuleta mipango itayoendana na hio Slogan
0 comments:
Post a Comment