Tuesday, November 24, 2015



NDESAMBURO ATOA MASHARTI MAGUMU CHADEMA.

Mdhamini mkubwa wa CHADEMA mh. Ndesamburo atoa masharti magumu kwa chadema baada ya Binti yake Lucy Owenya kukosa Ubunge wa viti maalum.


Ndesamburo alimwita Mbowe Moshi na kumpa masharti makali kuwa kama Binti yake Lucy Owenya hatapata Ubunge atasitisha misaada na kuipeleka kwa @ACTwazalendo kumuongezea nguvu Zitto Kabwe na kutangaza rasmi Vita na chadema.
Mbowe aliomba radhi na kuwatupia zigo Tume ya Uchaguzi ndio waliofanya makosa jambo ambalo sio kweli. Ndesamburo alimfokea Mbowe aache uhuni wake wa kumdanganya kuwa yeye sio mgeni na yeye kuisingizia tume makosa aliyofanya kwa makusudi.

Baada ya mazungumzo yote walihitimisha kwa kukubaliana. Mbowe aliomba radhi na kukubali kuyatekeleza masharti, kwa kuanza kumtoa Lucy Owenya nafasi ya 39 na kumshusha hadi nafasi ya 37 ya orodha ya mpangilio wao wa viti maalum . Nafasi ya 37 inamfanya Lucy kuwa mtu wa Kwanza katika viti maalum vipya watakavopata chadema baada ya kumalizika uchaguzi huu unaoendelea desemba 20. Kama tutakumbuka tume ya Uchaguzi walibakiza viti vitatu kutovigawa ndio hivyo ambavyo wanategemea kimoja wampe Lucy endapo wataongeza asilimia za kura za kupata sifa kupata viti maalum hivyo.

Hongera yako Lucy Owenya kupewa matumaini na poleni madada wa CHADEMA ambao mlikuwa nafasi ya 37 na 38 Lucy Owenya kupoka nafasi yenu na nyie kama Baba zenu ni wakubwa waambieni wakatoe masharti magumu kwa Mbowe.
Mpigakura wa kijijini Namalizia kwa kutumbua jibu kuwa kilichomkosesha Lucy Owenya nafasi ya kiti maalum na kuanza pigwa vita ndani ya chadema ni ukaribu wake na Zitto Kabwe, kama tutaendeleza siasa hizi za chuki tusitegemee kama tutafika na kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli.

Karama Kaila @Facebook

0 comments:

Post a Comment