Thursday, November 12, 2015



RADIO SWAHIBA KUFUNGIWA NA SERIKALI ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekifungia kituo cha Radio Swahiba FM kurusha matangazo yake, baada ya kutangaza matokeo aliyotoa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Cuf, Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), akidai alikuwa mshindi katika uchaguzi uliyofanyika Oktoba 25, mwaka huu visiwani humo.
 


Uamuzi wa kufungiwa kituo hicho cha radio ulitolewa jana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Chande Omar, kupitia barua ya Novemba 11, mwaka huu.
“Tume kwa kuzingatia uungwana uliotumia wa kukiri kosa na baada ya kupitia maombi yako kwa mujibu wa kifungu cha 16(3) na kifungu 3(F) imetoa tahfifu ya kutopokonywa leseni na badala yake kufungiwa hadi Januari 13, mwaka,” ilisema barua hiyo kwenda kwa kituo hicho cha radio.
 

Chande alisema pamoja na adhabu hiyo, mmiliki wa kituo hicho anatakiwa kueleza kwa maandishi kuwa kituo chake hakitarudia tena kosa kama hilo au jingine linaloweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
Alisema iwapo kituo hicho kitashindwa kujirekebisha pamoja na kupewa adhabu hiyo kwa kutumia kifungu cha 16 cha Sheria ya Tume ya Utangazaji ya Mwaka 2007, adhabu kali itachukuliwa.

0 comments:

Post a Comment