Saturday, November 21, 2015


"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar
Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake.


Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia.
Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa.
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma".-Zitto Z Kabwe

1 comment:

  1. Nampongeza sana na nina muheshimu ingawaje nikiri anautonesha sana moyo wangu anapoisemea vibaya CCM . Ningetamani kama kuna uwezekano wa mr zito ya kuwa miongoni mwa jeshi la magufuli atakaloliunda katika baraza lake la mawaziri. Ukawa walikuwa wakitafuta sababu ya fujo bungeni hiyo issue ya Zanzibar ni muhimu kila mpenda haki na amani angependa kuona inapatiwa ufumbuzi lakini kwa ukawa waliichukulia hiyo issue kama excuse yao ya kuhalalisha vitendo vya kishenzi katika siku ambayo watanzania wengi wanaichukuliya kama mwanzo mpya wa Tanzania. Sheni alikuwa mgeni mwalikwa tu maslahi ya watanzania zaidi million 40 na ushee ya watu waliokuwa Tanzania bara ni mapana zaidi ukilinganisha na wale waliokuwepo Zanzibar. Hata kukitokea matatizo Zanzibar ya kukimbia makazi yao basi Tanzania bara inayo uwezo wa kuwatafutia makazi wanzanzibar wote bila ya wasi wasi, sasa niambie kama Zanzibar inauwezo wa kuwatafutia makazi angalau wakaazi wa mkoa mmoja wa Tanzania bara,? Hapo utaona jinsi gani ukawa walivyo na watu wasio makini. Kwa kweli ukawa wanatakiwa kumuomba radhi mueshimiwa magufuli. Vile vile ukawa wanatakiwa kuwa makini na magufuli kwani ni mtu ambae watanzania wanaemkubali vitendo vyovyote vya kihuni zidi yake ni kujijengea uadui zidi ya wananchi.

    ReplyDelete