Posted by Williammalecela.com on Friday, November 27, 2015
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo mkoani DodomaBunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanyia mabadiliko makubwa sheria za
utumishi wa umma kwa kuondoa ajira za kudumu serikalini, ili kuwezesha
mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dk. John Magufuli.Katika
mabadiliko hayo mfumo sasa wa ajira za serikali kuwa za kudumu
utabadilishwa na badala yake, kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea
juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa uzembe uliodumu miaka nenda
miaka rudi, katika sekta ya umma.Akizungumza katika mahoajino binafsi na
Raia Mwema, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, alisema baadhi ya sheria
za kazi zinawafanya baadhi ya watumishi wa umma kuwa wazembe.“Kwa mfano
katika serikali ya sasa mfanyakazi mzembe kabisa kabisa hata waziri
kumfukuza kazi hawezi. Hata Katibu Mkuu hawezi mpaka afuate mlolongo
mrefu na hatua nyingi sana, yaani kazi ni guarantee (uhakika) katika
nchi yetu ni permanent and pensionable (ya kudumu na ina pensheni).
Sheria za namna hiyo lazima ziondoke,” alisema Spika Ndugai katika
mahojiano ambayo yamechapishwa ukurasa wa 12 wa gazeti la Raia
Mwema.“Katika nchi ambazo zinaendelea kwa haraka moja ya jambo ambalo
huna uhakika nalo ni ajira, ukifanya vizuri unayo ajira yako ukiboronga
unaondoka saa hiyo hiyo na wakati huo huo, sasa sheria za namna hiyo ni
lazima zibadilishwe ili watu wachape kazi. Wawe wakijua kabisa kwamba
nipo kwa sababu nachapa kazi akileta uzembe kazini kwaheri,”
aliongeza.Aliongeza kuwa mabadiliko mengine ambayo Rais Magufuli
atayaleta ni pamoja na ile sheria ya ununuzi na sheria nyingine ambazo
ni za hovyo hovyo, zinazoifanya serikali isifanye vizuri. Kwa mujibu wa
Ndugai, Bunge litahakikisha sheria hizo zibadilishwa haraka.“Huo ndiyo
ushirikiano wetu tutakaompa lakini pia tutachangia vizuri katika mipango
na bajeti zinazokuja tutazitengeneza vizuri zaidi kwa kupunguza fedha
zote za ulaji ulaji, hii ya kila mwaka mapazia, kuweka makochi, kuweka
makapeti na kompyuta kila mwaka na ofisi ni zile zile watu wale wale,
bajeti ilikuwa imejaa ununuzi wa magari vilainishi lazima tukate kote
huko,” alisema.Akizungumzia hatua hiyo, Rais wa Shirikisho la Vyama wa
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba, alisema hawezi kuunga
mkono au kukataa hoja hiyo mpaka atakapoona hoja yenyewe na maelezo
yake.“Kwa kawaida muswada wa sheria huanzia kwanza kwa wadau,
wakituletea tutaona, siyo kila kitu ni kibaya, sheria zinapotungwa
zinakuwa na sababu kwa nini zimetungwa. Unaweza ukawa na maelezo mazuri
tukajadili utekelezaji wake, tutaamua,” alisema.Alipoulizwa kuhusu
mwenendo wa baadhi ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa mazoea na kama
sheria hiyo inaweza kutibu tatizo hilo, alikiri kuwepo kwa hali hiyo
miongoni mwa watumishi wa umma lakini akatahadharisha kwamba tiba yake
siyo kuondoa ajira za kudumu.“Ziko sababu nyingi zinazosababisha baadhi
ya wafanyakazi kuwa wazembe, siyo ajira ya kudumu peke yake. Kama kwenye
nchi yenu mmeamua kubaguana kwa malipo, mmoja analipwa mara 30 ya
mwingine, huyo anayelipwa kidogo hawezi kuwa na morali ya kazi,
atanyong’onyea.“Yule anayepata mara 30 ataathiriwa utendaji wake na hawa
wenye kidogo kwa sababu ni wengi, kwa sababu watajifanya (wanaolipwa
kidogo) na serikali itajifanya inalipa lakini kumbe kinacholipwa
hakitoshelezi chochote,” alisema Mukoba.Aliogeza kwamba miaka ya 1970 na
1980 watu walikuwa na uhakika wa ajira za kudumu lakini walikuwa
wanachapa kazi kwa bidii kwa kuwa kulikuwa na uwiano wa haki kwenye
malipo ya mishahara, tofauti na sasa, akishauri pia suala la kushuka kwa
morali ya kazi miongoni mwa watumishi wa umma lifanyiwe utafiti makini
na si kulikurupukia.Chanzo: Raia Mwema print
0 comments:
Post a Comment