Wema
Sepetu (katikati), Idris Sultan upande wa kulia na kushoto ni Mh.
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji wakipata picha ya
pamoja katika jukwaa hilo la kulia ambalo lilikuwa maalum kwa wageni
mbalimbali waalikwa na watu maalufu ndani na nje leo wakati wa tukio la
kuapichwa kwa Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[TEMEKE-DAR
ES SALAAM] Wakati Watanzania na dunia nzima leo Novemba 5, 2015)
imeshuhudia kuapishwa kwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, Mastaa wanaotikisa Bongo na
wanapenda kufuatanafuatana kama kumbikumbi, Staa na mrembo, Wema Sepetu
‘Madam’ na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris
Sultan wametokea kuwa kivutio baada ya uwapo wao katika shughuli hiyo ya
kihistoria ndani ya uwanja wa shamba la Bibi.
Modewji
blog iliwashuhudia mastaa hao tokea waliposhuka kwenye gari na kisha
kuingia kwenye viunga vya uwanja huo wa Bibi, Wakati wa kuwasili kwa
wawili hao hali ya mvua ilikuwa ndio inataka kuanza hata hivyo walifika
uwanjani na kukuta uwanja umejaa sehemu za wageni waalikwa na kutulia
kwa mvua pembeni kabla ya kupatiwa nafasi ya kuketi.
Kwa
mujibu wa watu waliokuwa karibu na mtandao huu walinong’oneza kuwa,
Wawili hao licha ya kuonekana kuwa nadhifu na umaarufu wao, lakini
wameweza kukaa na kujichanganya na watu wengine wa kawaida na kuendelea
na shangwe za kumpongeza Dk. Magufuli.
Hata
hivyo, kadri ya uwepo wao huo kwenye jukwaa hilo la kulia linalotazama
uwanja, wakati walipoingia kukaa, walipata shangwe kubwa ya kushangiliwa
na umati mkubwa wa watu huku wengine nao wakishangilia pasipojua
wanashangilia nini.. hali hii iliweza kukusanya watu wengi zaidi kwenye
jukwaa hilo huku wengi wao wakifika kwa lengo la kuwashuhudia kwa macho
huku wengine wakipiga ‘Selfies’ za mbali ilimradi kuweka kumbukumbu zao.
Kitu
cha ziada kabisa kutokea uwanjani hapo ni baadhi ya vijana wa jeshi
waliokuwa karibu na jukwaa hilo kukodolea macho mara kwa mara kwenye
jukwaa hilo la akina Wema na Idrisa huku baadhi ya wanajeshi hao
walisikika wakinong’onezana na kuonyesha mahala alipokuwa amekaa Wema.
Hakika
hii ilikuwa ni kitu cha kipekee kwani wengi wa wananchi wakiwemo vijana
wa kike walivutika kufika kwenye jukwaa hilo ikiwemo hata kukaa kwa
mbali ilimradi tu wamshuhudia Wema na hali hiyo ilijidhihirisha kwani
hata walipoondoka baadhi yao nao waliondoka katika jukwaa hilo.
Hii
inaonyesha picha halisi kwani awali wasanii mbalimbali walifika kwenye
jukwaa hilo lakini hawakupata shangwe zozote wala watu kuwafuatilia ila
ujio huo pekee wa wawili hao uliibua shangwe za kushangilia na
kufuatiliwa mara kwa mara na hata kupiga picha na ‘fans’ wao.
Tukio
la kihistoria la Dk. Magufuli kuapishwa lilivyokuwa katika jukwaa
maalum leo Novemba 5, katika uwanja wa zamani wa Taifa maarufu Shamba la
Bibi.
0 comments:
Post a Comment