Monday, November 23, 2015

cur

Je unahesabu japo kwa vidole vyako kila kinchotokea katika ligi ya kikapu nchini marekani NBA? Kama jibu ni hapana basi amini kuwa Golden State Warriors chini ya kocha Luke Walton anayeshikilia kwa udamajukumu ya Steve Kerr waowanahesabu tena wa uhakika.

Kila wanachokiwaza mpaka sasa ni rekodi wanazoweka, na makubwa wanayoyafanya katika NBA. Inawezekana kabisa kuwa wanawaza kuweka rekodi ambayo watakufa wakiiacha ikisimama na vijukuu ndo washuhudie ikivunjwa. Lakini ukweli ni kuwa wanawaza mbali ya hapo, wanawaza kushinda kila siku tu.
Klay Thompson alifunga pointi 21, na kuiongoza Golden State Warriors kufikia rekodi ya kuanza msimu vizuri zaidi katika historia ya NBA,  kwa kuifunga Denver Nuggets 118-105 siku ya Jumapili usiku na kufikia rekodi ya 15-0.
Golden State Warriors wamefikia rekodi ya mwanzo bora wa msimu iliyokuwa inashikiliwa na  Washington capitols waliyoweka msimu wa  1948-1949  na ile ya msimu wa  ’93 -94 iliyowekwa na Houston Rockets . Warriors wanaweza kuvunja rekodi na kuweka yao Jumanne usiku nyumbani dhidi ya Los Angeles Lakers.
” Ni aina ya imani na utulivu tuliyonayo sasa  kwamba hakuna  anayehisi  kama tunakwenda kupoteza mchezo wakati wowote hivi karibuni ,” Stephen Curry alisema. “Njia sahihi ni sisi kucheza, maana tunaamini kuwa  tunaweza na tutakuwa bora zaidi. ”
Hiyo ni dhana ambayo inaogopesha kidogo, kwa kuzingatia hii timu imetoka kuvunja rekodi ya msimu wa  ’57 -58 iliyyowekwa na Boston Celtics kwa mabingwa watetezi kuanza kwa bora msimu na kushinda michezo mingi ambao wao walishinda michezo 14-0.
“Wao ni timu bora duniani, ni kazi ngumu kuwazuia. ” Alisema Nikola Jokic , ambaye alikuwa na pointi 11 na 11 rebounds kwa Nuggets. “Katika baadhi ya maeneo ya mchezo , tunaweza kujilinda , na katika sehemu nyingine , hakuna.
Namaanisha wanahitaji dakika tatu au nne na unawakuta wapo mbele kwa pointi 15, hivyo tunahitaji kucheza ulinzi wakati wote. ” Darrell Arthur alikuwa na pointi 21 kwa Nuggets , ambao wamepoteza michezo mitatu mfululizo.

0 comments:

Post a Comment