Monday, November 30, 2015

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja akiongea na wafanyakazi kwenye mkutano na wafanyakazi 
Ule usemi maaarufu wa Hapa kazi tu” unaendelea kuimbwa na kufanyiwa kazi na watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli.
Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na  wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.
“lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” aliongeza Luhemeja
Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi apate huduma ya Maji kihalali.
Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale aliposema “LAZIMA TUWATUE KINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo kwa maeneo stahili.
wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Afisa mtendaji Mkuu kwenye mkutano na wafanyakazi wote makao makuu ya shirika hilo Gerezani



0 comments:

Post a Comment