Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Siku chache zilizopita baada ya Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kutangazwa, Tanzaniatunatarajia Dk John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatangaza rasmi baraza lake la Mawaziri. Kila sekta itakuwa imeshikiliwa na Mawaziri ambao Rais ameridhishwa nao katika kukidhi viwango vya kuendesha sekta hizo na katika kurudisha matumaini ya watanzania.
Kati ya Wizara muhimu zinazokuza uchumi wa nchi kwa kasi ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii. je waziri mpya wa awamu ya tano atakuwa na uwezo wa kukabiliana na rushwa, ujangili na kuweza kuthamini maliasili na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii?
Miaka miwili iliyopita tumeshuhudia itikadi mbalimbali na kauli mbiu zilizofanya vizuri kuhimiza wananchi katika kuzuia ujangili, kati ya kauli mbiu zinazoendelea mpaka hivi sasa ni pamoja na “Tembo nao wanahisia”, hata hivyo bado kuna idadi kubwa ya watanzania ambao hawajatambua maana ya kauli mbiu hizi au umuhimu wa kutunza wanyama pori na iwapo watawajua watu wanaofanya ujangili ni wapi wataweza kuripoti matukio kama hayo. Je tunatarajia Waziri mpya atakaye jali na kuokoa wanyamapori?
“Kwa upande mwingine, baraza jipya la Mawaziri ndani ya utawala wa Magufuli litambue kuwa wawekezaji wengi katika sekta ya hii si wazawa au watanzania, ila ni watu wanaotoka nchi za jirani na nje ya bara la Africa. “tunatarajia waziri ataleta mabadiliko katika kuongeza idadi ya wawekezaji watanzania”, Andrea Guzzoni Meneja Mkazi waJovago Tanzania alifafanua
Mr. Guzzoni aliongezea kwa kusema kuwa sekta ya utalii bado haijaleta mchango mkubwa kwa watanzania katika upande wa kuongeza ajira au nafasi za uwekezaji, iliweza kuleta jumla ya 12% ya ajira kwa mwaka 2013 ambapo pia ilitarajiwa kushuka kufikia mwishoni mwa mwaka 2015 na kupanda kidogo kwa 2% ifikapo 2024. Tunatumaini baraza jipya la mawaziri litaleta nguzu na fursa nyingi za ajira kwa watanzania.
Hata hivyo, ukusanyaji wa kodi umekuwa ukifanyika bila mpangilio ambapo imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa vishoka wanaokula kodi za serikali, na kuongezeka kwa kiwango cha rushwa. “Ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha kodi zinalipwa kihalali, hivyo iwapo Waziri atakuwa anapinga vitendo hivi kwa kuchukua hatua Tanzania itaweza kukuza uchumi wake kwa muda mfupi”. alifafanua.
Asilimia kubwa ya wakazi hawajui umuhimu wa utalii wa ndani, ni muhimu kutambua mali tunazomiliki kwa kuwa ni vigumu kupeperusha bendera ya utalii katika nchi za nje iwapo sisi wenyewe hatujafahamu faida ya mali tulizomiliki.
0 comments:
Post a Comment