KIJANA Juma
Rajabu mwenye umri wa miaka 15, mwenyeji wa Manyoni mkoani Singida yupo
katika maumivu makali, kufuatia ugonjwa wa ajabu uliompata katika mguu
wake, ambao anadai chimbuko lake hasa ni ajali ya kugongwa na gari
iliyompata wakati akitokea dukani.
Akiwa
hana wazazi wote wawili waliofariki akiwa bado na umri mdogo, Juma
anasimulia jinsi alivyokutana na ajali hiyo inayomsababishia mateso
kwani ili atibiwe, zinatakiwa fedha ambazo yeye binafsi hana.
“Nilikuwa
nimetumwa dukani kukununua vitu, wakati narudi nyumbani ndipo likatokea
gari likanigonga. Badala ya kusimama, dereva akakimbia eneo la tukio na
kuniachia mzigo huu mkubwa.
“Tangu
nilipopata ajali hii, sikuwahi kupata matibabu, mguu unazidi kuoza tu,
nikalazimika kutoroka kutoka Singida na kuja hapa Dar, ambapo napo sina
ndugu wala msaada wowote. Nilipofika sikuwa na mwenyeji, nikalazimika
kufikia Posta ambako ninalala kwenye vibaraza.
“Licha
ya maumivu, mguu wangu unabadilika kila siku, nilijaribu kwenda
Hospitali ya Mwananyamala, ambako waliniambia ili nitibiwe ni lazima
niwe na fedha, kuna wakati nilifikiri hali hii inatokana na mguu wangu
kuota tende, lakini nimeambiwa siyo tende bali ni kutokana na uchafu
maana tangu nigongwe sijawahi kufanyiwa usafi wowote,” anasema kijana
huyo huku akibubujikwa na machozi.
Kwa
yeyote aliyeguswa na hali ya mtoto huyu na anajisikia kumsaidia,
anaweza kumpa msaada wowote kupitia nambari 0788 061199 au 0713 380581,
ambazo ni za askari anayemsaidia, Titasi Balili.
0 comments:
Post a Comment