WAZIRI MKUU
Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu
ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
“Ofisi ya
Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku
za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Alitoa kauli
hiyo jana mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na
wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es
Salaam.
Jana ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
"Pamoja na
kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na
ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata
mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini
ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka
vipaumbele vyetu sawa,” alisema.
Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo
imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu
kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema ana
imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa
wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi
karibuni.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, NOVEMBA 23, 2015.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu,
Majaliwa Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia ofisini
kwake , Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)

Baadhi ya
watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa
Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha
, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Majaliwa Kassim Majaliwa akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Dkt. Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi
ya Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha
kwa watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt.
Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa
kujitambulisha alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

0 comments:
Post a Comment