MWIGIZAJI wa kike wa Filamu anayefanya vizuri Bongo Jennifer Ernest ‘Leila’ amefunguka kwa kusema kuwa rushwa ya ngono na dhuluma katika tasnia ya Filamu inaua vipaji halisi na kubaki wababaishaji wanaopewa nafasi kwa ajili ya kujitoa sadaka ya miili yao.
Leila anasema kuwa watayarishaji wengi wamekuwa wakitolea muswada (Script) katika mahoteli au nyumba za kulala wageni na waopewa ni wale wanaokidhi matakwa yao, lakini mbaya zaidi ni wasanii kuchezeshwa kwa mikopo ambayo kulipwa ni bahati.
“Usione kuna wasanii wanaonekana kila filamu, kuna mambo mawili tu, rushwa ya ngono au kucheza bure, mimi sipo tayari kwa ajili ya hilo, najiheshimu, najipenda na wala sipo tayari kuigiza kwa ajili ya kuuza sura,”anasema Leila.
0 comments:
Post a Comment