Sunday, November 1, 2015

Ndoto Zangu Zimefika Kimataifa– Godliver
NYOTA wa filamu ya Aisha na tamthilia ya Siri ya Mtungi Godliver Godian ‘Aisha’ amefunguka kwa kusema kuwa ndoto zake ambazo amekuwa akipigania toka kuanza kwake kwa sana anaona sasa zimefunguka kwa kushiriki katika kazi kubwa akianzia na Siri ya Mtungi na filamu ya Aisha.

Nashukru Mungu kwa kunifungulia milango nimepigana sana katika tasnia ya filamu na lengo kuu ilikuwa kucheza filamu kimataifa na nimefikia huko baada ya kucheza sinema kubwa kama Aisha ni hatua kubwa sana baada ya kufanya vizuri katika Siri ya Mtungi,”anasema Aisha.
Msanii huyo ambaye ameigiza katika filamu kubwa ya Aisha kuzinduliwa katika jumba la sinema la Mlimani City na kurushwa siku kumi huku ikiwa ni kivutio kwa wapenzi wa filamu waliofika na kuiona , filamu hiyo imetayarishwa na Kijiweni Production chini ya muongozaji Amil Shirvji.
Chanzo: GPL

0 comments:

Post a Comment