Sunday, November 15, 2015

Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali.

Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.

Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.SOMA ZAIDI>>>

1 comment:

  1. mburula tu na kushindwa maisha wanafikiri wakiwa wanawake ndio watayapatia maisha lo!! poor them..

    ReplyDelete