Thursday, November 26, 2015

KWANINI NAKWAMBIA TAFUTA MWANAUME SIO MVULANA.
 
1.Mwanaume anapoishi, Pana Muonekano wa “Nyumbani” sio “Nyumba” yaani sio lazima awe na mali nyingi, wala si lazima iwe nyumba yake. Jambo la msingi ni je, anajali makazi yake? Hata kama anaishi chumba kimoja, je, chumna chake kipo katika Mpangilio..? Ukienda kwake ni saa kumi lakini ukakuta kitanda hakijatandikwa na vyombo alivyotumia kwa chakula bado vipo Mezani. Uyo ni Mvulana Mpe nafasi awe Mwanaume.


2.Mwanaume ana Malengo ya Maisha na Kufanya anachokipenda bila kujali anakutana na changamoto gani. Mwanaume mwenye ukomavu kiakili siku zote anamipango ya kutoka hatua A kwenda B na kuna kitu cha ndani kinachomvuta afanye hivyo.

3.Mwanaume anauwezo wa kujitegemea kimaisha, na yeye mwenyewe kiujumla. Yaani hata kama amelewa hategemei mtu ampeleke nyumbani. Na hata akipata ofa kutoka kwa rafiki zake huthamini fedha ya rafiki zake. Hanywi sababu ananunuliwa ila hunywa kama ananunua yeye.

4.Mwanaume ana Msimamo na mipaka yake, Si kila utakachomuambia anakubaliana nacho. Ukiona unamwambia Twende club yeye anakubali, Twende beach anakubali tu.. Huyo ni Mvulana Mpe Muda akomae.

5.Mwanaume Siku zote anajua anataka nini, vipaumbele vyake maishani, na wewe ni mmoja wa vipaumbele hivyo. La sivyo unaishi na Mvulana si Mwanaume

6.Mwanaume Hakuambii Huwezi siku zote, Mwanaume wa kweli anakupa moyo, na anamuda wa Kukusaidia kutimiza ndoto zako, anajua mahitaji ya mpenzi wake na kuyatengea Muda Fulani.

7.Hufanya Maamuzi, japo haoni tatizo kukuacha ufanye baadhi ya maamuzi pia.

8.Anajua Thamani yako, Hakuambii tu anakupenda, bali hukuonyesha ni jinsi gani anakupenda.

9.Hakuonei aibu, Si msumbufu na huamini juu ya upendo wenu na si mtu wa kuchat chat kila saa au kupigs simu kila dakika. Ukiona anapenda kuchat kila saa bby tuchat Jua hana Malengo huyo ni Mvulana bado mbichi Muache akomae.

10. Anajipenda, anajituma, Anavaa na kufanya mambo kiutu uzima na ana malengo yake ya baadae.

0 comments:

Post a Comment