Jukwaa likiwa limepambwa.
Wapiga gitaa maarufu nchini, John Kitime na Anania wakifanya yao.
MWANAMUZI maarufu wa Soukous kutoka Kinshasa nchini Kongo, Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba, yupo Tanzania kufanya shoo kwenye Tamasha la Muziki wa Asili ya Kiafrika lijulikanao kama, Karibu Bagamoyo Music Festival 2015, ambalo limeanza kurindima katika Viwanja vya Mwanakalenga mjini Bagamoyo, Pwani leo.
Tamasha hilo limekutanisha watu wazima na watoto. Usiku wa leo mkongwe huyo wa muziki, Papa Wemba anatarajia kufanya shoo kubwa katika tamasha hilo.
Tamasha hilo litaendelea kufanyika mpaka Novemba 9 mwaka huu.
PICHA NA DENIS MTIMA/ALIYEKO BAGAMOYO
0 comments:
Post a Comment