STAA wa Ngoma ya My Woman My Everthing kutoka nchini Nigeria, Patrick
Nnaemeka Okorie ‘Patoranking’, usiku wa kuamkia leo amewasha moto wa
hatari katika Fukwe za Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Katika usiku huo uliotambulika kama Friday Night Fever, Patoranking
alisindikizwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva akiwemo msanii zao la
Endless Fame, Mirror ambaye alianza kupanda jukwaa hilo na kukonga
nyoyo za mashabiki hao.
0 comments:
Post a Comment