Rais
wa Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza kuwa ana $150,000 (£100,000)
kwenye akaunti zake za benki, katika hatua inayolenga kuendeleza uwazi
na kupiga vita ufisadi serikalini.
Bw Buhari anamiliki makao matano na nyumba mbili za matope,
pamoja na mashamba kadha, akaongeza.
Kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi alichaguliwa kuwa rais mwezi Machi ahadi zake kuu zikiwa kukabiliana na ufisadi na ukosefu wa usalama
Ufisadi ni tatizo sugu katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika na mwezi uliopita, Bw Buhari alisema $150bn (£100bn) zimeporwa kutoka kwa hazina ya serikali.
Buhari ana shamba la matunda na renchi yenye ng’ombe 270, kondoo 25, farasi watano na ndege wengi.
Taarifa hiyo ilisema Bw Osinbajo ana $900,000 (£600,000) kwenye akaunti zake za benki. Kwenye fomu ya kutangaza utajiri wake, Bw Osinbajo pia alifichua anamiliki nyumba nne.

0 comments:
Post a Comment