Tuesday, November 10, 2015

Dr. Magufuli jana akitoa tai yake kabla ya kuwavuruga wazembe Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Magufuli pia anatazamiwa kufanya mabadiliko makubwa ya:-
Wizara nane kufutwa zingine kuunganishwa.
Imefahamika kuwa rais Magufuli ameamua kupunguza ukubwa wa serikali yake kwa kufuta wizara 8 kati ya wizara 28 zilizokuwepo, habari haijataja ni wizara zipi zitakazopunguzwa.

Je hii inamaanisha nini?? Ni kwamba mawaziri 8 na manaibu 8 watapungua, makatibu wakuu wa wizara 8 hawatakuwa na nafasi hiyo tena, magari 16 ya mawaziri na manaibu wake pia magari 8 ya makatibu wakuu ambayo jumla yake yatakuwa 24 yatarudishwa sehemu nyingine ili kuhudumia watanzania.

Serikali itapunguza matumizi yake yaani mishahara na marupurupu ya mawaziri na manaibu na makatibu wakuu haitakuwepo.

0 comments:

Post a Comment