Posted by Williammalecela.com on Tuesday, November 17, 2015
 |
Leo ni siku muhimu kwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John
Pombe Magufuli. Siku ya leo uundwaji wa Serikali utaanza. Kuundwa kwa
Serikali kutatanguliwa na kuchaguliwa kwa Spika, kuapishwa kwa Wabunge,
kuchaguliwa kwa Naibu Spika na na kuidhinishwa kwa Waziri Mkuu.
Kikatiba,mawaziri huteuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.
Mawaziri na Manaibu Mawaziri watakaoteuliwa ndio watakaotoa taswira na
ueĺekeo wa Serikali ya Rais Magufuli. Watakapoteuliwa Mawaziri na
watendaji wengine,Tanzania itaanza safari na mwendo wa awamu ya tano.
Hakika, leo ni siku ya kuandikwa kwa ajili ya kumbukumbu. |
0 comments:
Post a Comment