Shoga, ni matumanini yangu kwamba upo mzima na unaendelea na maisha
baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao ulikuwa na changamoto nyingi
na kutuweka mioyo juu kwa presha ya kupanda na kushuka.
Shoga yangu, katika maisha hakuna mtu ambaye hapendi kuwa na kitu kipya, jambo hilo halipo na kama yupo basi mtu huyo atakuwa na tatizo f’lani.
Kikubwa shoga ni kumaliza tofauti zetu za kisiasa kwa sababu Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ( Nec) imemtangaza Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais
Mteule wa Awamu ya Nne wa taifa letu.
Baada ya kusema hayo ngoja nirejee kwenye jambo ambalo nimekuandalia
linalokutaka kuwa mpya kila siku katika ndoa yako ili kumdhibiti mumeo
atulie nyumbani kwa sababu ukizembea tu wenzio watambeba jumla.
Shoga yangu, katika maisha hakuna mtu ambaye hapendi kuwa na kitu kipya, jambo hilo halipo na kama yupo basi mtu huyo atakuwa na tatizo f’lani.
Nasema hivyo kwa sababu hata nguo zetu zinapopauka au kuchakaa huwa
tunaacha kuzivaa na kununua mpya lengo likiwa ni tupendeze.Linapokuja
suala la mapenzi, kila mtu hupenda mwenza wake awe mpya asiyechosha
wanapokuwa kwenye uwanja wa fundi seremala.
Upya ninaouzungumzia ni mwanamke aliyeolewa kujiongeza katika kila
idara kuhakikisha muda wote mumewe anamuwaza na kumdhibiti asiwawaze
michepuko.Mwanamke lazima uwe mbunifu wa mambo ya chumbani zaidi kadiri
siku zinavyokwenda mbele, jua namna ya kumdekea mumeo, kumbembeleza na
kumhamasisha kimalovee ili kila wakati awe na hamu ya kuwa nawe.
Mhamasishe mumeo kwa kumvalia nguo za mitego muwapo wawili chumbani
au nyumbani kwani akiiona shepu yako ‘tamu’ ni wazi atakupa raha mtoto
wa kike.
Huo ndiyo upya ninaouzungumzia badala ya kuvaa nguo ndefu
zilizokuziba mwili wote vaa nguo nyepesi ambazo zitaonesha kila kitu
kilichomo mwilini mwako kwani mumeo umepewa na Mungu jiachie utakavyo
mwana kwetu ili afurahi. kisha akufurahishe pia. Bye


0 comments:
Post a Comment