Tuesday, November 24, 2015

Amani Vincent (kulia) mwenyekiti wa klabu ya Stand United ya mjini Shinyanga

Amani Vincent (kulia) mwenyekiti wa klabu ya Stand United ya mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa klabu ya Stand United Amani Vincent amelalamikia shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuingilia mambo ya ndani ya klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuiandikia barua  klabu hiyo ili isajili wanachama na kufanya uchaguzi wa viongozi haraka.


“Kwanza naomba niseme klabu yangu ya Stand United haina mgogoro kwa maana ya kwamba hakuna ugomvi kwenye kamati ya utendaji au kwa wanachama isipokuwa tunashangaa uhalali wa TFF kusema kwamba tunamgogoro na kutuandikia barua ya tarehe 4 November 2015 barua ikitoka kwa katibu mkuu inayohusu mgogoro wa Stand”, amesema Vincent.

“Barua inamaelekezo na nitayasoma hapa baadhi ya maagizo hayo: “Yafuatayo ni maagizo mnayotakiwa kutekeleza ili kufikia tamati ya mgogoro huo ambao ni mgogoro sadikika”, kwa kushirikiana na kamati ya uendeshaji ambayo hiyo kamati ya uendeshaji kupitia kwa mkuu wa mkoa, TFF wanatuagiza tuandae fomu za maombi ya uanachama na wadau waanze kuchukua fomu hizo kunzia tarehe 5 hadi 20 November 2015 fomu hizo zitakuwa kwenye vituo viwili, ofisi ya katibu mkuu Stand na kamati ya uendeshaji”.

“Kwanza kuambiwa sisi tuna mgogoro inatuletea usumbufu na mdhamini kwa maana ya kwamba, mdhamini atakaposikia kuna mgogoro wa aina yeyote inaweza kutuletea madhara kwa mdhamini”.

“Sasa sisi kama wanachama, TFF wao wametuagiza haya na wao wanasema kuanzia tarehe hizo tuwe tumetoa fomu kitu ambacho wanakuwa wameinyang’anya kamati ya utendaji mamlaka yake kwa mujibu wa katiba yetu lakini pia wanatoa tarehe 3 mpaka 5 December kwa maelezo yao wanatarajia mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF atatangaza uchaguzi wa Stand United”.

“Hii ni kinyume na katiba yetu na katika hili tunasema kwamba hatuungani mkono na TFF na tunaishangaa TFF kubariki vitu kama hivi ambavyo ni kuuyumbisha huu mpira”.

0 comments:

Post a Comment