Posted by Williammalecela.com on Friday, November 06, 2015
 |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete leo Jumatano, Novemba 4, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo
na Katibu Mkuu wa Chama cha Civic United Front (CUF), Mheshimiwa Seif
Shariff Hamad ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa chama
hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 25.
Viongozi hao wawili walikutana kwa kiasi cha saa moja Ikulu, Dar es salaam, kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kufuatia ombi la Mheshimiwa Hamad kutaka kukutana na kuzungumza na Rais Kikwete.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa mashauriano yaendelee kufanyika
baina ya pande zote zinazohusika na hali ya kisiasa Zanzibar.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015
|
0 comments:
Post a Comment