Martin Kasyanju enzi za uhai wake.
Mmiliki
wa Bendi ya FM Academia, Martin Kasyanju amefariki dunia jana akiwa
Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Msemaji
wa Bendi ya FM Academia, Kelvin Mkinga amethibitisha kutokea kwa msiba
huo na kusema kuwa Martin amefariki akiwa katika Hospitali ya Aga Khan
jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa takribani wiki mbili.
Kwa
mujibu wa Kelvin ni kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa
malaria lakini baadaye ikagundulika kuwa ana ‘Pneumonia’ (Nimonia).
Msiba
upo nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Mahenge, Oysterbay jijini Dar na
mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii katika makaburi ya
Kinondoni jijini Dar.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.
0 comments:
Post a Comment