Mtihani mkubwa walionao wasanii wachanga ni kufikia level za wasanii waliotangulia ambao kwa sasa wengi wao wamekuwa wakifanya video za gharama kubwa na waongozaji wa nje ya Tanzania.
Rapper wa Arusha, Gentriez amesema wasanii wengi wamekuwa wakiumia kuona wenzao wakitengeneza video kubwa zinazochezwa kwenye video vya runinga vya kimaitafa wakati wao hawana uwezo huo.
Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Gentriez alisema wasanii wengi hawana uwezo hata wa kumlipa Hanscana kufanya naye kazi na wanaposikia wenzao wakienda mbali zaidi ya hapo wanazidi kupata uchungu.
Amesema ni kazi ngumu kwao kwenda sambamba na wasanii wanaokimbia wakati wao ndio wameanza kujifunza kutambaa.
0 comments:
Post a Comment