Tuesday, November 24, 2015

Image copyright
AFP
Image captionCharles de Gaulle





Polisi wa Ufaransa wanatathmini kile kinachoaminika kuwa ni mkanda wa kujitoa muhanga, uliopatikana kusini mwa nje ya mji wa Paris

Watu wanaokusanya taka ndio waliokiona kitu hicho katika pipa la taka huko Montrouge.

Vyanzo vya polisi vinasema, kitu hicho kinafanana na mikanda iliyotumika katika mashambulizi ya mjini Paris, ambayo ina sehemu ya mbele na ya nyuma ya kuwekea chaji.
Pia inachunguzwa ila kubaini iwapo mkanda huo ulivaliwa na mshukiwa mkubwa Salah Abdeslam.
Wakati huo huo, kwa mara ya kwanza Ufaransa, imepeleka vikosi vyake kupambana na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu IS kupitia ndege yake ya Charles de Gaulle.

0 comments:

Post a Comment