Friday, November 27, 2015

Adele 25
Adele Laurie Blue Adkins, anayefahamika zaidi kwa jina lake la kwanza ni muimbaji kutoka Uingereza ambaye ameshatoa album tatu mpaka sasa.


Adele 25

Kuna kitu kimoja ambacho binafsi nilijiuliza na kuamua kufuatilia, kuhusu majina yake ya album zake zote tatu kuwa namba. Album ya kwanza aliita ’19’, iliyofata inaitwa ’21’, na hii mpya ya mwaka huu inaitwa ’25’, hizi namba zina maana gani?

Jibu ni kwamba namba ambazo Adele amekuwa akizitumia kama majina ya album zake ni umri wake.

Adele-19

Wakati anaanza kurekodi album ya kwanza mwaka 2007 alikuwa na umri wa miaka 19, japo album hiyo ilitoka mwaka uliofata 2008 akiwa na miaka 20.

Print

Album ya pili alianza kuirekodi mwaka 2009 akiwa na miaka 21, na ilikuja kutoka miaka miwili baadae mwaka 2011 akiwa na miaka 23.

Album mpya iliyotoka November 20, 2015 alianza kuitayarisha mwaka 2013 alipokuwa na miaka 25, lakini imekuja kutoka mwaka huu akiwa na miaka 27.

Hivyo majina hayo ni umri aliokuwanao kipindi anaanza kurekodi album husika.

“I was 20 when 19 came out. I was 23 when 21 came out. I am 27. And so proud of being 27, thanks very much…But I quite liked it when I was 25.” alisema Adele

Hivi karibuni alipokuwa akipromote album mpya, Adele alisema ‘25’ ndio itakuwa album ya mwisho kuipa jina la umri wake.

“I think this will be my last age one. I’m sure I’m wrong with this but I feel there’s been a massive change in me in the last couple of years.”


0 comments:

Post a Comment